![]() |
DON BOSCO LIONESS ...CHAMPS 2016/17 |
![]() |
SAVIO,,,CHAMPS 2016/17 |
Klabu ya mpira wa vikapu ya Savio ya Upanga, Don Bosco jijini Dar es salaam imechukua ubingwa wa taifa.
Hii ni baada ya kuifunga timu ya jeshi ABC vikapu 77 kwa 66 kwenye fainali iliyofanyika jumapili ya tarehe 15 ndani ya uwanja wa taifa wa mpira wa vikapu.
Amini Mntambo wa Savio mwenye jezi namba 14 ndiye mchezaji bora wa ligi.
Michuano hiyo ilianza tarehe 7 Mei 2016 na jana jumapili ndiyo ilikuwa ni kilele chake.
Savio kwa mara ya kwanza walishiriki mashindano haya yaliyofanyika Tanga mwaka 2005 ambapo fainali walikutana na timu ya jeshi ya JKT na kuwafunga.
Savio kupitia ligi hii ya taifa wameshachukua ubingwa huu zaidi ya mara 5.
Walichukua ubingwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2009/2010, 2010/2011, 2011/2012.
Sasa wamefuzu kucheza Zone 5 na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti. (BBC)
0 maoni:
Chapisha Maoni